Kisa cha Jongoo na Nyoka : Hadithi za Watoto 2019
Na: Queen Haji
FUNDISHO- Tujitahidi kuwa wa kweli katika maisha,uongo ni jambo baya.
Hapo zamani za kale, Jongoo na Nyoka walikuwa marafiki
wakubwaa sana kiasi kwamba watoto wa jongoo waliweza kwenda kwa nyoka wakacheza
Wakaishi huko nakurudi Nyumbani bila matatizo.
Enzi hizo Nyoka alibarikiwa kuwa na miguu Jongoo akapewa
macho na Mwenyezi Mungu, basi Nyoka na
Jongoo waliendelea kuwa marafiki lakini waliishi vijiji tofauti.
Siku moja Nyoka alipata mualiko akahudhurie harusi ya Kuku
lakini sharti waalikwa wote lazima wawe na macho ili waweze kuwaona maharusi na
kusheherekea vyema katka harusi hiyo, Jongoo na familia yake hawakupata mualiko
basi Nyoka akawaza akakumbuka kuwa yeye ana miguu sasa ataendaje kwenye harusi?
ikabidi aende kijijini kwa rafiki yake Jongoo Kabla ya harusi ili akamuazime macho.
Basi alipokwenda Jongoo akamkaribisha kwa furaha Nyoka, Nyoka akamuomba
jongoo amuazime macho Jongoo akagoma akambembeleza sana, basi Jongoo akampa
masharti kama unaomba macho lazima na wewe uniachie miguu ili nipate hata kutembea
kwakupapasa kama unavyofanya wewe, basi nyoka akaona isiwe tabu akampa na yeye
akachukua macho.
Kwakua nyoka hakuwahi kuona katika maisha yake yote alivopata
macho alishangaa sana vitu vilivyomo duniani akafurahi kweli, basi akaenda
kwenye harusi akasheherekea kwa furaha zote.
Baada ya harusi Nyoka akaona macho ni bora zaidi kuliko
miguu yake hakurudisha tena macho kwa Jongoo na Jongoo alivoona kimya aliumia
sana na hakuweza kufanya lolote kwakua hakuweza kuona tena.
Hadithi yetu ikaishia hapo ndomana hadi Leo nyoka anatembea
kwa tumbo lakini anaona na jongoo ana miguu ila hakuweza kuona tena.
FUNDISHO- Tujitahidi kuwa wa kweli katika maisha,uongo ni jambo baya.
Kisa cha Jongoo na Nyoka : Hadithi za Watoto 2019
Reviewed by HISTORY
on
April 26, 2019
Rating:
No comments