MALKIA WA BARAFU (HADITHI YA MTOTO)
Kulikuwa na binti aliyeishi maeneo
ya jangwani,binti huyu alikuwa ni mwerevu,mwenye upendo,mwenye hekima na
aliyemsaidia kila mtu kwa jambo lililo ndani ya uwezo wake,na binti huyu
aliitwa Samantha.
Siku moja aliingia bibi kizee mmoja
ambaye aliomba apewe chakula hata kidogo,Samantha alimpa bibi yule chakula.Baada
ya kumaliza chakula aliomba maji lakini kwa sababu ni jangwani hapakuwa na
maji.Yule bibi kizee akasema “nashukuru mjukuu wangu na ili kuonesha shukrani
zangu kwako nakupa zawadi”.Kisha akampa mkufu ung’aao zaidi ya dhahabu na
kumwambia “kwa kuvaa mkufu huo utakuwa ni Malkia wa barafu kwani utakuwa na
uwezo wa kushusha barafu na kuamuru maji nayo yakakutii”.Kisha bibi yule
akatoweka huku akiacha harufu nzuri ndani ya nyumba ile.
Samantha aliamua kuuvaa mkufu ule
ghafla akawa na uwezo wa kushusha barafu.Malkia huyu wa barafu alikuwa ni kam
kito cha thamani katika jangwa lile kwani aliwasaidia wote kwa kuwapa maji na
wakaishi kwa furaha siku zote zilizofuatia.
*********MWISHO***********
MALKIA WA BARAFU (HADITHI YA MTOTO)
Reviewed by HISTORY
on
August 17, 2018
Rating:
No comments