MBWA WA AJABU (HADITHI YA MTOTO)
Kulikuwa na familia aliyoishi
baba,mama na watoto wao watatu wa kiume pamoja na mbwa wao.Siku moja ilimbidi Baba aende vitani kwasababu alikuwa ni mwanajeshi. Aliwaaga mke na watoto wake
lakini pia aliandika wosia ili kama asipofanikiwa kurudi wasigombane kutokana
na mali.
Baada ya muda kupita bila kupata
taarifa yoyote kutoka vitani alipoenda Baba yao, Mama aliamua aende akamuangalie Baba yao kama anahitaji
msaada wowote lakini kwa bahati mbaya alikuta Baba amefariki,kutokana na mshituko wa Moyo,Mama nayeye akafariki hapohapo.
Watoto walipata taarifa kuwa Mama yao na Baba yao wamefariki dunia na wamezikwa kwa heshima zote za kijeshi.
Waliamua kuangalia wosia ulioachwa na wazazi wao na kukuta imeandikwa kwamba mtoto wa kwanza atapata nyumba wanayoishi, mtoto wa pili atapewa shamba na mtoto wa tatu atapewa mbwa waliekuwa naye.

Maisha yaliendelea lakini mtoto wa
tatu hakuwa na kitu chochote cha kula na cha kumpa mbwa wake, zaidi ya kipaji chake
cha kutunga mashairi. Lakini mbwa alisema kama ukiweza kunipa mfuko na majani
yanayotumika kama chakula kwa wanyama utauona umuhimu wangu,yule mtoto akaamua
ampe mbwa kitu anachohitaji.
Mbwa yule baada ya kupewa anachohitaji alienda eneo la msituni lenye sungura wengi akaweka majani kwenye mfuko wa majani na kuweka karibu na shimo lenye sungura kisha kulala pembeni kama amekufa. Baada ya muda mchache waliingia sungura wanne kwenye ule mfuko aliwakamata na kuwapeleka kwa mfalme.
Alipofika alisema Mwalimu wangu wa mashairi ameleta hii zawadi kwa ajili yako mfalme,Mfalme aliipokea zawadi kwa mikono miwili lakini alijiuliza sana huyu Mwalimu wa mashairi ni nani?

Mbwa yule aliendelea kupeleka zawadi
mbalimbali kwa mfalme na jambo hilo lilizidisha udadisi kwa mfalme kuhusu
Mwalimu wa mbwa huyo mwerevu.
Siku moja Mbwa mwerevu aligundua kwamba mfalme na mwanae wa kike walikuwa wakisafiri kwenda kuona maeneo mbalimbali ndani ya nchi yake. Mbwa akaenda upesi kwa Mwalimu wake akamwambia aende akakae kwenye mto kama anataka kuzama huku akisubiri likipita gari la mfalme aombe msaada.
Lilipopita gari la mfalme mbwa alipiga kelele akisema "msaada, msaada, Mwalimu wangu wa mashairi anazama jamani msaada” kwakuwa Mfalme analijua lile jina vizuri akawatuma walinzi wake wakamsaidie.
Alipookolewa hakuwa na mavazi ya kuvaa kwani mavazi yake yalikuwa yameloa, hivyo akapewa mavazi ya Kifalme, alipendeza sana na alionekana mtanashati katika mavazi hayo ya kifalme, binti wa mfalme ndiye aliyemwambia hivyo wakati wakiwa njiani kuelekea nyumbani kwa Mwalimu.

Katika mji
alioishi mtoto huyo kulikuwa na gofu lisilotumika na mtu, mbwa yule aliamua
kulipamba, aliposikia gari ya mfalme ikikaribia alitoka kuwakaribisha huku
akisema "karibuni katika nyumba ya Mwalimu wangu wa mashairi tunayoishi mimi na yeye kama familia moja
kwani hana ndugu mwingine zaidi yangu". Baada ya binti wa mfalme kusikia hivyo
aliona huruma alimuomba baba yake, yeye na Mwalimu waoane kwani ni Dhahiri
kwamba wanapendana hivyo mfalme hakuwa na pingamizi.
Siku ya siku
ikawadia ndoa ikafungwa wakati wa zawadi alikuja kijana aliyejitambulisha kama
mtu aliyewakutanisha binti wa mfalme na Mwalimu wa mashairi lakini hawakuamini
kwani yule alikuwa ni mbwa, ghafla alibadilika na kuwa mbwa waliyemzoea na
kurudi katika hali yake ya ubinadamu na kuanza kusimulia "Baba yetu alikuwa na
watoto wanne lakini mimi nilikuwa ni mgonjwa na njia pekee ya kupona ilikuwa ni
kuishi kama mbwa na ndiyo maana nikaachwa kwa mtoto wa mwisho kwani ndio ana
upendo wa kweli” Mwalimu alishukuru sana kumpata ndugu yake na wakaishi kwa
furaha siku zote zijazo.
***********MWISHO************
MBWA WA AJABU (HADITHI YA MTOTO)
Reviewed by HISTORY
on
August 17, 2018
Rating:
Waooh gd job
ReplyDelete