Ads Top

JICHO LA USALITI









SURA YA KWANZA

Ilikuwa ni siku ya jumapili yapata saa 2:45 asubuhi, mimi na mdogo wangu   Jane tulikuwa tumemzunguka mama yetu mpenzi aliyekuwa amelala kitandani akitaabika na ugonjwa, tulikuwa tupo katika shauku kubwa ya kutaka kujua mama yetu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa gani.baada ya muda mfupi daktari alifika wodini kuzungumza na mama.

Daktari: habari za asubuhi,

Mama: salama dokta

Mimi Na Jane: shkamoo dokta

Daktari: Marahaba watoto wazuri naomba mngoje nje kidogo niongee na mama sawa?

Mimi Na Jane: sawa daktari

Baada yakuondoka daktari akaanza kuongea na mama

Daktari: Mama unatatizo la saratani ya shingo ya kizazi, ambalo limesababishwa na virusi viitwavyo Human papilloma (HPV).

Mama: ooh! Mungu wangu

Dokta: kinga yako ya mwili ilishindwa kuondoa hayo maambukizi, chembe hai za kawaida zikaanza kukua bila mpangilio na kusababisha dalili za awali za saratani, lakini nasikitika hukuzijua dalili hizo mapema.

Mama: ooh, kwaiyo ndio nimeisha kufa tayari babaangu?

Daktari: hapana mama tutajitahidi kukuhudumia vizuri, usipate hofu.

Mama: Mungu wangu nisaidie mimi!

Daktari: kuna njia tatu ambazo hapa hospitali tuna zimudu njia ya kwanza ni Trachelectomy hapa manaake tunaitoa shingo ya kizazi nakubakisha mfuko wa uzazi kwaajili ya uzazi hapo siku za baadaye. Njia ya pili ni Radiotherapy tunatumia mionzi kutibu saratani iliyosambaa, na tatu ni chemotherapy hii ni njia ya dawa za vidonge na sindano. Kwahiyo mama hapo ni wewe tu kuchagua njia ambayo unaona kwako ni naafuu.

Mama: bora vidonge na sindano daktari

Daktari: Sawa mama, kwa sasa tunaupungufu wa dawa hizo, na pia wataalamu wa njia zingine nao huwa tunaazima toka hospitali ya sant George, hivyo matibabu tutaanza rasmi kesho kutwa, sasa hivi utahamia katika chumba maalumu kwa ajili ya uangalizi maalumu ukisubiri siku ifike.

Mama: sawa daktari nimekuelewa,

CHUMBA MAALUMU-JIONI

Kama kawaida yetu Mimi na mdowangu Jane tulikuwa tupo na mama tukimzunguka na kumfariji taratibu, muda huu mama kwa huzuni alikuwa akituangalia kwa macho makini sana kana kwamba anatafakari jambo fulani, akaniita.

Mama: Ian mwanangu

Ian: ndio mama

Mama: Tangu Baba yenu afariki dunia miaka miwili iliyo pita kwa ajali ya basi, koh...Koh...koh, nimekuwa ndiye mlezi pekee niliye baki, sindio mwanangu?

Ian: ndio mama!

Mama: basi kuanzia sasa wewe ndio mlezi mpya wa dada yako

Jane: mamaaaa! Kwanini unasema hivyo?

Mama: mh! Jane mwanangu kua uyaone

Baada yakusema hayo mama alimtazama Jane akamshika mashavuni na mikono yake miwili, kisha akatoa tabasamu hafifu lililo jaa upendo mkubwa. Muda wote huo nilikuwa nikitoa machozi kimyakimya huku nikimtazama mama bila kupata majibu ya swali langu kwamba naota au nikweli.

Mama: Jane binti yangu

Jane: ndio mama angu

Mama: kimbia dukani Kwa mzee kibotro kaninunulie maziwa ya maji nahisi njaa

Jane: sawa mama

Baada ya Jane kuondoka tu, mama alinitazama usoni bila kukwepesha macho Kwa sekunde kadhaa, kisha akasema

Mama: Ian mwanangu, unamiaka 17 sasa ushakuwa mkubwa, hatakama wenzako wa umri huo bado wanakuwa chini ya uangalizi wa wazazi wao, lakini sikuzote matatizo huleta uzoefu ambao ni faida katia jamii na pia tambua vidole havilingani

Ian: ndio mama najitambua

Baada yakusema hivyo nilijipangusa pua iliyokuwa ikivuja majimaji

Mama: Dada yako Jane bado mdogo Sana ingawa anaakili Sana za kuzaliwa, lakini miaka yake ni 12 tu hivyo anahitaji uangalizi wakaribuu Kama…………

Ian: Kama nini? Kama nini mama? Mbona unaongea kama mtu anaye aga, unampango wa kwenda sehemu kuugulia mama? mbona daktari kasema uvute subira wakija hao wataalamu utapata matibabu.

Niliongea kwa uchungu sana huku nikilia kama mtoto mdogo

Mama: Ian mwanangu, mtu yeyote Yule, haidhuru awe mbali vipi na shughuli za kisayansi, mapambano ya kisiasa, harakati za kimapinduzi, na kadhalika, huwa na hamu ya kutaka kujua vile ulimwengu utakavyokuwa kwa wakati ujao.

Akatulia kidogo kisha akaendelea

Mama: mwanangu mpenzi

Ian: ndio mama

Mama: malimwengu yamzungukayo mwanadamu hayana kikomo wala mipaka yoyote ile na hatimaye kujaa siri ambazo mwanadamu anaweza kuzigundua kwa taratibu tu, hatua kwa hatua, lakini hatafaulu kamwe kuzijua zote kwa ukamilifu.


BOFYA MAANDISHI HAYA KUENDELEA KUSOMA
JICHO LA USALITI JICHO LA USALITI Reviewed by HISTORY on May 27, 2019 Rating: 5

No comments