SIWEZI KURUDI
SEHEMU YA KWANZA
(EPISODI YA KWANZA)
Unaonekana mji wa
wastani,watu wakipita katika njia ndogondogo zenye mashimo ya hapa na pale,miti
na maua vikitoa harufu tamu mithili ya marashi toka nchi za mbali,pembeni ya
mji huo wanaonekana wafanyabiashara wadogo wadogo ambao wameweka bidhaa zao
katika vibanda vilivyo jengwa katika ubora hafifu na kuezekwa mabati
kuukuu,kelele za hapa na pale zinatoa tafsiri nzuri ya mji wa waswahili.
(Zina sikika
kelele-hamaki na taharuki)
Watu: Uyo! Uyo! Kamata,
piga (hahahahahaaa) mkate ngwara,kibaka uyooooooo!
Mwanamke wa kwanza:
(kwa sauti ya huzuni) Maskini! Wakimkamata watamuua kijana wawatu, naogopa ata
kuona wakimkamata.
Mwanamke wa Pili:
jamani! Hebu ona, afu ni kijana mzuri tu,shababi kabisa harafu anakuwa mwizi.
Mungu wanusuru watoto wangu jamani.
Katikati ya njia
nyembamba anaonekana kijana wa makamo akikimbia na kuvuruga utaratibu wa
biashara,anaruka matunda ya wauzaji,anadondosha bidhaa chini,uso wake umechakaa
jasho na makunyanzi ya hofu,mtetemo wa mdomo mithili ya kitambaa kinacho
peperushwa na feni. Nyuma yake wanaonekana vijana wanne walio shiba kweli kweli
wakimfukuza kijana huyo na kumfanya alete shida katika soko la Machinjioni.
Kijana mmoja anawaacha
kwa mbio mita kadhaa wenzake watatu na kumkaribia mtuhumiwa,anamkaribia karibu
na kumpiga mtama,anafanikiwa kumwangusha chini, anamrukia na kumkalia
tumboni,anampiga na kiganja cha mkono usoni,anampiga ngumi.
(watu
wanakusanyika-hamaki na taharuki zikiendelea)
Vijana watatu nao
wanafika eneo aliloangushwa kijana anaefukuzwa,wanaungana na mwenzao
kumshambulia kijana aliyechini.
Watu: (wakishangilia)
Piga uyo! Kata mayai kanga! Tumewachoka vibaka hapa sokoni mpunguze uyo! (sauti
ya mwanamke- vuruga kabisa uyo,tengua kiuno icho)
Kijana aliyechini
(anayepigwa) anafanikiwa kujikung’uta na kuwaachia shati lililo chanika wale
vijana wanne,anapenya katikati ya kundi la washangiliaji na kupokea makonde
kadhaa kutoka kwa baadhi ya wananchi wasiojua hata kosa lake,anafanikiwa
kushika njia tena,anakimbia!anakimbia maskini! Gafla anamparamia dada wawatu
aliyesimama pembeni akizungumza kupitia simu yake.
Vuuuuuup! Chini,wote
wawili.
Dada: ooh! Mungu
wangu,utaniua we kaka! (kwa sauti iliyobanwa)
Wanasogea haraka
wanaume wawili walio valia suti zao safi na vifaa masikioni na kumuinua dada
huyo,wanaonekana ni walinzi.
Mlinzi mmoja: (Kwa
hofu) pole bosi,umeumia?
Mlinzi wa pili:
Puuu,(akimrushia konde kijana ambaye bado yupo chini akijizoa zoa,kutokana na
maumivu aliyopewa na watu wenye hasira kali.)
Dada: Muache tafadhari!
Msikilize imekuwaje.
Gafla! Wale vijana
wakafika katika eneo la tukio, wakisindikizwa na wananchi wapambe,wasio na kazi
za kufanya,wapenda matukio wenzangu,mkononi smartphone tu,pyaa pyaaa video
zinachuliwa ndugu! Mzunga wa shangwe kama wote,mambo motoo hatari.
Wakaanza kumshambulia
tena Yule kijana, (huku wale walinzi wakimzunguka Yule dada na wakiwa wanamtoa
katika eneo la tukio) Yule dada akafoka.
Dada: msaidieni!
Msaidieni na waambia!
Walinzi wakawatawanya
wale vijana wanne waliokua juu ya kijana aliekuwa akifukuzwa na kumsaidia.
Kijana wa kwanza:
Mwachie uyo! Mwachie uyo! ( huku akihema kwa nguvu) mwizi uyo,kabeba PC yangu pale hosteli,ina research yangu,mwachie
uyo!
Kijana Mwizi: (huku
akihema kwa hofu) mnisa-sa-samehe jama-jama-jamani, Dada naomba mnisaidie,mnipeleke
apo mtaa wa pi-pili nikawape PC yenu,sa-samahani jamani!
Dada: (kwa sauti ya
ukali) kumbe umeiba kweli!
Mwizi: kweli Dada,kweli
Dada angu,nisaidie tu,kikombe hiki kinipite,ntakupa sababu
baadae,tafadhari,tafadhari sana.
Baada ya kijana mwizi
kupokea tena kipigo cha makonde kadhaa licha ya walinzi kumsaidia,waliafikiana
na kuingia kwenye gari la binti chini ya uangalizi wa walinzi binafsi na kwenda
mtaa wa pili,kijana mwizi alikabidhi kompyuta ya wale wanafunzi wa chuo,lakini
pia Dada alitoa fedha kadhaa kama pole kwa wale vijana na kuwaomba wasifike
mbali zaidi.
Vijana waliondoka na
kutokomea upande wa mashariki. Dada,walinzi pamoja na kijana mwizi nao
waliondoka pamoja kwenye gari na kuelekea nyumbani kwa wazazi wa Yule Dada.
NYUMBANI SEBULENI
Zinaonekana samani za
kifahari katika ukumbi wa wastani,mapambo mbalimbali yanayo toa tafsiri ya
kipato cha Yule Dada. Kijana mwizi anaonekana kukaa katika moja ya makochi pale
ukumbini,wakati walinzi wakiwa wamesimama katika pande kadhaa wakiimarisha
ulinzi. Dada anapandisha ngazi na kuelekea vyumbani.
Baada ya muda
mfupi,anarudi akiwa amevalia suruali ya jinsi,pamoja na tisheti ya kijivu isiyo
mbana,anasogea na kukaa karibu na kijana mwizi.
Dada: (huku akimtazama
mwizi usoni,kwa jicho la kustaajabu) Naitwa Mwana,mkurugenzi wa shirika la
ndege la Eagle na mfanyabiashara maarufu wa mafuta. Mh! Enhee na wewe
mwenzangu.
Mwizi: Naitwa
Faraja,kazi yangu mwizi
Mwana: (huku akijizuia
kucheka) sasa unaletaje Faraja kwa kazi yako ya wizi,mh! Tangulini Faraja akawa
mwizi my dear.
Faraja: maisha na
changamoto zake zinapelekea kutenda nje ya matamanio ya walio tupa majina, (akainamisha
kichwa chini,baada ya muda akainua tena,akamtazama kwa makini Mwana,kisha
akasema) Dada, samahani na njaa kali sana.
Bila hiana Mwana
aliinuka na kumkaribisha Faraja mezani, meza imesheheni vyakula vya kila
aina,nyama,mbogamboga,matunda nakadharika kana kwamba kuna sherehe ya mwana
mfalme kumbe ni mlo wa siku tu. Faraja alikaa kiti cha upande wa kushoto na
Mwana alikaa mbele yake lakini ni upande wa pili, walinzi sita walionekana
kusimama na kuupamba ukumbi ule kwa mitutu ya bunduki, wahudumu wakionekana
kuingia na kutoka ukumbini.
Faraja alishika kisu
mkono wa kulia na uma mkono wa kushoto,alionekana mahiri sana wa kutumia vitu
hivi tofauti na sifa zake,kitu ambacho kilimpa mashaka Mwana.
Mwana: Faraja,naweza
kujua elimu yako tafadhari? (huku akimtazama machoni)
Faraja: Kidato cha nne,
( huku akionesha kutojali na kuendelea kufakamia chakula)
Mwana: unanidanganya!
Faraja: kwanini?
Mwana: ungekuwa
umeishia kidato cha nne,ungejibu nimefika form four,lakini jibu lako umelijibu
kisomi zaidi kana kwamba unafahamu vizuri namna ya kujibu lakini pia rafudhi
yako inaonesha umeelimika zaidi. Kuwa wazi naweza kukusaidia Faraja!
Faraja: hoja yako
dhaifu dada
Mwana: (huku
akistaajabu) whaaaaat! We kaka,mbona unajikuta hivyo.
Gafla,Faraja akarusha
kisu alicho kuwanacho mkononi na kumchoma mlinzi mbele yake, akapanda juu ya
meza na kuzunguka akitumia matako,mkononi akishika uma ana tambaa kwa haraka na
kumchoma na uma machoni mlinzi wa pili.
Wakati huo Mwana alikua
chini ya meza,akipiga yowe la ajabu! Faraja alichukua silaha ya mlinzi aliye mchoma
na uma jichoni na kuanza kujibizana risasi. Wakati mapigano yakiendelea
anaonekana mlinzi mmoja akimlenga Mwana chini ya meza, Faraja anabinua kochi na
kulitumia kujikinga na risasi huku akilisukuma kochi kuelekea upande alio
kuwepo Mwana na kumnyakua kisha kumsogeza karibu yake. Ziliendelea kurindima
kelele za risasi kwa pande zote mbili lakini umahili wa Faraja uliweza
kuwaangusha walinzi wote chini.
Faraja alimuinua Mwana
aliyekuwa akitetemeka mwili mzima,hofu kuu machoni pake huku mikono yake
ikitetemeka kama jenereta. Walianza kuondoka kuelekea mlangoni,kabla Faraja
hajafungua mlango mlinzi mmoja amliyekuwa hajafa aliinua mtutu wake kwa tabu na
kumpiga Mwana risasi ya kifua! kisha mlinzi huyo akaanguka na kukata roho.
Faraja alipagawa,Mwana
kamwangukia,mikono ya Faraja imejaa damu, Mwana akilalamika.
Mwana: nakufa! Nakufa!
Faraja umeniua,U-umeniua, u-u-u-meniua sina kosa mi-mi
Baada kusema maneno
hayo,alinyama kimyaa!
Faraja: (huku
akimtingisha) Madame!madame! madameeeeeeeee! (Kilio)
******************kimya**********
SIWEZI KURUDI
Reviewed by HISTORY
on
May 28, 2019
Rating:
No comments